Skip to content
PPP TV
THE FEED ⚡

Cardi B Afichua Kwa Nini Hataki Kubaki Single Maisha Yake Yote

EMBy Eugine MicahPPP TV Newsroom · Nairobi · 24 Jul 2026, 09:36 EATCardi B Afichua Kwa Nini Hataki Kubaki Single Maisha Yake Yote

Rapa maarufu wa Marekani, Cardi B, amewajibu mashabiki wanaomtaka aendelee kuwa single na kujikita katika maisha yake binafsi, akisema hana mpango wa kubaki bila mpenzi maisha yake yote. Akizungumza kupitia Spaces kwenye mtandao wa X, Cardi alisema kuwa alikuwa single kwa kipindi chote cha ziara yake ya muziki na hakuwahi kuzungumza wala kutoka kimapenzi na mtu yeyote. “Nitakuwa single milele?

Haiwezekani. Nahitaji pia kuwa na mtu wa kuniburudisha,”alisema Cardi, akieleza kuwa baada ya kuachana na nyota wa NFL Stefon Diggs ameendelea kufurahia maisha kwa kusafiri, kutoka na marafiki na kupumzika. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 33 alikiri kuwa kutokana na umaarufu wake, analazimika kuwa makini zaidi katika kuchagua mtu wa kuwa naye na kwamba inamchukua muda kuamini na kumpenda mtu.

“Labda naweza kuchagua wanaume bora zaidi, inawezekana. Lakini sitabaki single milele. Maisha ni mazuri, lakini hata moyo wangu unahitaji upendo,”alisema.

Cardi B alihusishwa hivi karibuni na nyota wa NFL Stefon Diggs, ambaye walipata mtoto wa kiume aliyezaliwa Novemba 2025. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kusuasua, huku Cardi akieleza mapema mwaka huu kuwa alipoteza imani kwake na kuamua kujikita zaidi katika kulea watoto wake, muziki na ziara zake za kimuziki. Hata hivyo, vyanzo vya karibu nao vilidai kuwa Diggs alifanya jitihada za kurekebisha uhusiano huo, jambo lililomfanya Cardi aanze kufikiria upya kuhusu mustakabali wao.

WHATSAPPPOST ON XFACEBOOK
YOUR BRAND HERE
Reach 2.5M+ Kenyans daily — advertise on PPP TV · info@triplep.tv
PPP TV NEWSROOM

Reported and written by the PPP TV Newsroom, Nairobi. © PPP TV — Powerful, Precise & Pristine.

MORE STORIES →
© 2026 PPP TV · Powerful, Precise & Pristine · StarTimes Ch. 430