Skip to content
PPP TV
THE FEED ⚡

Video: Dkt. Nchimbi Awataka Watanzania Kuweka Nguvu Kwenye Katiba Mpya

EMBy Eugine MicahPPP TV Newsroom · Nairobi · 24 Jul 2026, 15:28 EATVideo: Dkt. Nchimbi Awataka Watanzania Kuweka Nguvu Kwenye Katiba Mpya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kuwa Katiba ndiyo sheria kuu ya nchi yenye mamlaka ya kubatilisha au kufuta sheria yoyote inayokinzana nayo mara tu inapopitishwa, hivyo akisisitiza umuhimu wa kuweka kipaumbele katika mchakato wa kupata Katiba Mpya. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) uliofanyika leo Julai 24, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Dkt.

Nchimbi alisema badala ya kutawanya nguvu za kisiasa kwenye masuala madogo madogo, wananchi wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kupigania Katiba Mpya kwani ndiyo msingi wa mabadiliko na marekebisho mengine yote. Alisisitiza kuwa haki na amani haviwezi kutenganishwa, akieleza kuwa mtetezi wa amani hawezi kuwa adui wa haki, wala mtetezi wa haki hawezi kuwa adui wa amani. “Hakuna mashindano ya nani anaanza.

Haki ni msingi wa amani. Haiwezekani mtetezi wa amani akawa adui wa haki na mtetezi wa haki akawa adui wa amani. Hili halifikiriki, ni jambo ambalo ni muhimu tujiepushe nalo,”alisema Dkt.

Nchimbi. Makamu wa Rais aliongeza kuwa anatamani kuona Tanzania ambayo kila mwananchi atajivunia utaifa wake na kuishi katika mazingira yanayozingatia haki, umoja na amani kwa wote.

WHATSAPPPOST ON XFACEBOOK
YOUR BRAND HERE
Reach 2.5M+ Kenyans daily — advertise on PPP TV · info@triplep.tv
PPP TV NEWSROOM

Reported and written by the PPP TV Newsroom, Nairobi. © PPP TV — Powerful, Precise & Pristine.

MORE STORIES →
© 2026 PPP TV · Powerful, Precise & Pristine · StarTimes Ch. 430